Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bi.Ursula von der Leyen amesema, Umoja huo unafanya juhudi kufikia makubaliano ya kiwango cha juu ya biashara na Uingreza, na Uingereza inatarajiwa kuingia soko pekee la Umoja wa Ulaya.
Alizungumza katika mkutano wa bunge la Ulaya, Bi.Von der Leyen amesema, baada ya kufikia "azimio la kisiasa" na Uingereza, Umoja wa Ulaya umefanya juhudi kutimiza lengo la kufuta ushuru na kuondoa vizuizi vya kibiashara, hii ni njia mpya ya kufanya biashara ambayo haijatolewa na Umoja huo kwa wenzake wengine wa kibiashara. Lakini Bi. Von der Leyen pia amesisitiza kuwa, Uingereza lazima itekeleze jukumu lake na kufuata kanuni ya Umoja huo kama ikitaka kupata upendeleo maalumu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |