Wizara ya biashara ya China leo imesema, itaboresha zaidi huduma za vibali na maombi kwa maonyesho ya makampuni ya kigeni yanayohusiana na uchumi wa kiufundi na kiteknolojia.
Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo imesema, waombaji wanaweza kufuta au kubadilisha tarehe za ufunguzi za maonyesho hayo ya kigeni ambayo yameidhinishwa au kuwasilishwa kwa wizara ya biashara ya China kwa njia ya mtandao. Kuanzia Jumanne, vibali vya usimamizi vya maonyesho ya kiuchumi na kiteknolojia ya kampuni za kigeni yanayofanyika kwa mara ya kwanza nchini China yatatolewa kupitia mtandao.
Pia wizara hiyo imezitaka serikali za mikoa nchini China kuimarisha mawasiliano na wafanyabiashara muhimu katika sekta ya maonyesho, na kutoa sera ili kuwasaidia kupunguza hasara na kukabiliana na matatizo yoyote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |