Jamii ya kimataifa imepongeza hatua ya rais Xi Jinping wa China ya kufanya ziara ya ukaguzi wa kazi za kudhibiti maambukizi ya virusi vipya vya korona (COVID-19) mjini Beijing, na kusema ziara hiyo imeongeza imani juu ya vita dhidi ya COVID-19.
Msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Fadela Chaib amesema Shirika hilo linaunga mkono kwa dhati mapambano ya China dhidi ya virusi hivyo. Pia amesema, ziara ya rais Xi imetoa ishara muhimu kwa China na pia jamii ya kimataifa.
Naye mwenyekiti wa Klabu ya Kundi la 48 la Uingereza Stephen Perry amesema, kupitia ziara hiyo, rais Xi ameonyesha wasiwasi wake kwa wananchi wake, na nia thabiti ya kupambana na mlipuko huo.
Aliyekuwa naibu waziri mkuu wa Thailand Pinij Charusombat amesema, ziara ya rais Xi katika wakati huu muhimu imeonyesha kuwa serikali imetoa kipaumbele kwa maisha ya wananchi wake, na kutoa ujumbe kwa jamii ya kimataifa, kuwa watu wa China wameungana kwa juhudi za pamoja katika kukabiliana na tatizo hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |