Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Wang Yi atahudhuria Mkutano wa 56 wa mambo ya usalama utakaofanyika Munich nchini Ujerumani kuanzia tarehe 13 hadi 15 mwezi huu.
Geng amesema, Wang atahutubia mkutano huo, na kujibu masuala yanayofuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa, kueleza juhudi na matokeo ya serikali na watu wa China katika kupambana na maambukizi ya virusi vipya vya korona, na kuhimiza ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na maambukizi hayo kwa pamoja. Pia Wang atatoa maoni na mapendekezo ya China juu ya ushirikiano wa pande nyingi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.
Kabla ya mkutano huo, Wang na mwenzake wa Ujerumani Heiko Josef Maas watafanya mazungumzo ya kimkakati ya awamu ya tano juu ya mambo ya kidiplomasia na usalama kati ya China na Ujerumani mjini Berlin.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |