• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yashukuru jamii ya kimataifa kwa kuiunga mkono kukabiliana na maambukizi

  (GMT+08:00) 2020-02-12 18:21:43

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang ameshukuru jamii ya kimataifa kwa kuiunga mkono China kukabiliana na maambukizi ya virusi vipya ya korona COVID-19.

  Serikali ya Canada hivi karibuni imesema nchi hiyo haitaweka kizuizi dhidi ya Wachina kuingia nchini humo. Geng amesema China inapongeza uamuzi huo wa Canada, na huu ndio msimamo wenye busara na wa kisayansi.

  Russia, ambayo ni nchi mwenyekiti wa Kundi la BRICS, kwa niaba ya kundi hilo imetoa taarifa ya kuunga mkono juhudi za China za kukabiliana na COVID-19. Geng amesema taarifa hiyo inaonesha moyo wa nchi za BRICS wa kushirikiana na kushikamana katika kukabiliana na changamoto, na China ingependa kushirikiana kwa nguvu zote na jumuiya ya kimataifa ikiwa ni pamoja na Kundi la BRICS, na kupambana na maambukizi, ili kulinda usalama wa afya wa kikanda na kimataifa.

  Mawaziri wa afya wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya watafanya mkutano maalumu kuhusu maambukizi ya COVID-19, ili kuratibu hatua za nchi hizo. Mwezi uliopita, Umoja huo umetenga dola milioni 10 za kimarekani kutafiti virusi vinavyosababisha maambukizi hayo, na utaendelea kutoa misaada kwa China. Geng amesema China inaishukuru jamii ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Ulaya kwa kusaidia China kukabiliana na maambukizi hayo, na kupenda kuongeza mawasiliano na WHO na jamii ya kimataifa, ili kushinda maambukizi hayo mapema.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako