• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TFF kuivunja Kamati ya saa 72

  (GMT+08:00) 2020-02-12 18:23:20

  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema kuwa litaivunja Kamati ya Saa 72 ya shirikisho hilo kama watabaini kuna uzembe unaofanyika katika kutoa maamuzi. Kamati ya Saa 72, ikijulikana pia kama Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi, ni chombo maalumu kilichopo chini ya TFF na Bodi ya Ligi kinachoshughulikia masuala mbalimbali yanayohusu ukiukwaji wa kanuni na sheria ambazo zinaendesha ligi zote nchini, ikiwemo ishu za wachezaji, viongozi wa timu na marefa wa ngazi zote. Uamuzi huo unakuja mara baada ya kuibuka malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali wakidai chombo hicho kinachelewa kutoa maamuzi ya matukio mbalimbali yaliyotokea michezoni, huku baadhi ya matukio hayo yakishindwa kutolewa ufafanuzi licha ya kuonekana kuwa kuna makosa ya wazi yamefanyika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako