• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SADC yapiga kambi Tanzania kujadili sekta wanyamapori

  (GMT+08:00) 2020-02-12 18:59:42
  Maofisa wa sekretarieti ya Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wanaoshughulikia sekta ya wanyamapori na utalii wameanza majadiliano ya siku nne na Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori nchini Tanzania kwa ajili ya kuanzisha mafunzo maalum kwa mameneja na askari wa wanyamapori wa jumuiya hiyo.

  Ofisa wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori (Mweka), Ernest Emmanuel amesema maofisa hao wa SADC wako katika ziara ya siku nne kuanzia Februari 11 hadi 14 katika Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

  Timu hiyo inaongozwa na Ofisa Mwandamizi wa Programu ya Maliasili wa SADC, Deborah Kahatano ambaye amefuatana na Tawanda Gotosa, Mshauri wa Ufundi wa maeneo yaliyohifadhiwa yanayovuka mipaka ya nchi.

  Chuo hicho kimethibitisha kuwa wataalamu hao wa SADC pia wanalenga kupata ufahamu wa jumla kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na chuo hicho cha kimataifa.

  Hivi karibuni, Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania ilikipa jukumu Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka kutoa mafunzo maalum kwa waongoza watalii nchini.

  Mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha watoa huduma katika sekta ya utalii kupata sifa za kusajiliwa na kupewa leseni ya kuendelea kutoa huduma hiyo kwa mujibu ya Sheria ya Utalii Namba 11 ya Mwaka 2008 kifungu cha 48.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako