• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhaba wa chakula wabiasha hodi Kenya kufuatia mvua kubwa

    (GMT+08:00) 2020-02-12 19:00:21

    Huenda Kenya ikakumbwa na uhaba wa mahindi kufuatia mvua kubwa ambayo imeendelea kunyesha kote nchini Kenya. Wakulima wanasema mvua hiyo iliwazuia kuvuna kwa wakati mahindi yao jambo ambalo lilisababisha mahindi yao kuharibika shambani. Taarifa hii inakuja wakati ambapo idara ya utabirio wa hali ya hewa ya Kenya kusema mvua hiyo itaendelea kunyesha hadi mwezi juni. Tangazo hilo la idara ya utabiri wa hali ya hewa limewafanya viongozi katika maeneo yaliyoathiriwa kutafuta njia mbadala ya kuondoa chakula shambani wakati huu ambao mvua hiyo kubwa inaendelea kunyesha. Uvunaji wa mahindi mara nyingi hufanyika katika mwezi wa Januari katika maeneo mengi ya mkoa wa kati. Wataalam wanasema mahindi mengi huenda yakaoza kutokana na kuvunwa wakati wa mvua hali ya baridi.Aidha wataalam hao wamesema wanatarajia bei ya mahindi kupanda kutokana na uhaba wa mahindi.Wakenya wengi hupendelea kula ugali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako