• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WHO yatoa jina rasmi kwa ugonjwa wa virusi vipya vya korona kuwa ni COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-02-12 19:27:54

    Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa jina rasmi kwa ugonjwa unaosababishwa na virusi vipya vya korona kuwa ni COVID-19, na kusema kuwa chanjo dhidi ya virusi hivyo inaweza kuwa tayari ndani ya miezi 18.

    Tangazo hilo lilitolewa jana huko Geneva na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambaye alisisitiza umuhimu wa kuwa na jina rasmi la virusi. Alisema kuwa na jina kuna umuhimu katika kuzuia utumiaji wa majina mengine ambayo yanaweza kuwa sio sahihi au kusababisha unyanyapaa, jina hilo pia linasaidia kuwa na mfumo sawa wa kutumia ikiwa kutokea milipuko wa virusi vya korona.

    Habari zinasema, WHO imeandaa mkutano wa wanasayansi zaidi ya 400 duniani kutafuta njia za kukabiliana na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako