• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari 51 wa Syria wauawa katika shambulizi lililofanywa na jeshi la Uturuki mkoani Idlib

    (GMT+08:00) 2020-02-12 19:34:17

    Askari 51 wa Syria wameuawa katika shambulizi lililofanywa na Jeshi la Uturuki kaskazini magharibi mwa Syria, na kusababisha mvutano kati ya serikali za Syria na Uturuki kuwa mbaya zaidi jana.

    Mchunguzi mmoja wa vita amesema jeshi la serikali ya Syria limedhibiti barabara kuu kati ya Aleppo na Damascus. Habari kutoka kundi la waasi zinasema mapambano bado yanaendelea kaskazini mwa barabara ya M5, ambako wametungusha helikopta ya jeshi la Syria, na kuwaua rubani wawili.

    Uturuki imeonya kuwa, italipiza kisasi kwa jeshi la serikali ya Syria linaloungwa mkono na Russia kama likishambulia jeshi la Uturuki baada ya kupata maendeleo katika kuondoa ngome ya mwisho ya waasi. Nalo Jeshi la Syria jana lilisema litajibu shambulizi hilo la jeshi la Uturuki.

    Mjumbe maalumu wa Marekani nchini Syria Bw. James Jeffrey leo atakutana na ofisa wa ngazi wa juu wa Uturuki mjini Ankara, ambako watajadili jinsi ya kutatua mgogoro kwa njia ya kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako