• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkoa wa Xinjiang washuhudia wajasiriamali wapya 75,000 mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2020-02-12 20:09:06

  Idara ya nguvukazi na huduma za jamii ya mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, nchini China imesema, mwaka jana imezindua sera kadhaa na kuwasaidia watu 75,000 kuanza biashara zao wenyewe.

  Serikali ya mkoa huo imesema, imeongeza viwango vya mikopo kwa wakaazi wanaojiajiri na wafanyabiashara wadogo ili kupunguza shida zao za kifedha. Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa, mwaka jana, jumla ya wajasiriamali wapya 74,700 wametoa nafasi 144,300 za ajira. Pia serikali hiyo imeongeza ujenzi wa vituo vya kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili kurahisisha biashara na kuboresha ujuzi wa kitaalam kwa umma, haswa kwa wafanyakazi wahamiaji, wahitimu wa vyuo vikuu na wanajeshi waliostaafu. Kulingana na mpango wa serikali, Xinjiang itaendelea kuweka sera nzuri za kuongeza watu wengine 30,000 wanaojiajiri na kutoa nafasi 90,000 za ajira kwa mwaka 2020.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako