Emmanuel Adebayor amejiunga na klabu ya Olimpia ya nchini Paraguay akiwa mchezaji huru na kutangazwa siku ya Jumanne ya wiki hii. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal, Manchester City na Tottenham, hii inakuwa klabu yake ya 10 katika ulimwengu wa soka baada ya kumaliza kuitumikia klabu ya Kayserispor ya nchini Uturuki kwa miezi mitatu hadi mwezi Disemba. Nyota huyo raia wa Togo kwa sasa ana umri wa miaka 35, na kwa muda alihusishwa kujiunga na miamba hiyo ya soka ya nchini Paraguay baada ya rais wa timu hiyo, Marco Trovato kuahidi kumsajili mchezaji huyo. Olimpia kwa sasa ipo kwenye nafasi ya tano kwenye ligi kuu ya nchi hiyo maarufu kama Apertura ambapo kwa sasa Adebayor atakuwa pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Roque Santa Cruz.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |