Maandalizi ya Riadha za Dunia za mashindano ya mabingwa wa dunia ya vijana chini ya miaka 20 yamezidi kupamba moto wiki hii huku ujumbe wa viongozi kutoka makao makuu ya Shirikisho la Riadha Duniani huko Monaco ukiwasili nchini Kenya. Maofsa 19 wa Riadha Duniani wamewasili Nairobi juzi kwa ziara ya siku mbili ili kuangalia maandalizi ya michuano hiyo itakayofanyika Julai 7 hadi 12. Maofisa hao wanaotoka idara mbalimbali za Shirikisho la Riadha Duniani na washirika wao, wanatarajiwa kukagua hatua iliyopigwa na kamati ya maandalizi ya Kenya LOC. Rais wa LOC Jack Tuwei, amesema maofisa watakuwa na mikutano Jumatano na Alhamis kwa siku nzima na idara mbalimbali za kamati ya maandalizi. Mtendaji mkuu wa michuano hiyo ya mabingwa Myke Rabar, amesema ziara hiyo ni muhimu katika kuanzisha awamu ya mwisho ya maandalizi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |