• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • BAISKELI: Mwendesha Baiskeli wa Australia Kai Sakakibara awekewa dawa ya kulala baada ya kupata mejeraha makubwa ya kichwa

  (GMT+08:00) 2020-02-13 08:14:57

  Mwendesha Baiskeli wa BMX Australia Kai Sakakibara amewekewa dawa ya kulala baada ya kupata mejeraha makubwa ya kichwa kwenye mashindano ya kombe la dunia. Mwanaolimpiki huyo mwenye miaka 23 alidondoka kwenye raundi ya ufunguzi huko Bathurst, New South Wales siku ya Jumamosi. Alipewa dawa ya kulazwa hapohapo kwenye tukio kabla ya kuchukuliwa na kupelewa Hospitali ya Canberra, ambako alifanyiwa upasuaji kupunguza shinikizo kwenye ubongo wake. Sakakibara hivi sasa yupo namba 10 duniani na alimaliza wa tisa kwenye michuano ya mabingwa ya mwaka jana. Mdogo wake wa kike Saya pia ni mwendesha baiskeli wa BMX kwenye timu ya Australia akiwa na nafasi ya tano kwenye viwango vya dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako