Grand Prix ya China imeahirishwa rasmi jana kutokana na mlipuko wa virusi vya covid-19. FIA, imekubali ombi la waandaaji wa China kuahirisha mbio za Shanghai ambazo zilipangwa kutimua vumbi Aprili 19. Kwenye taarifa yake FIA imesema pande zote zitachukua muda wa kutosha kujadili tarehe mpya ya mbio hizo. Uamuzi huo umefikiwa ili kuhakikisha afya na usalama wa madereva, wafanyakazi na mashabiki. Grand Prix ya China imekuwa sehemu muhimu kwenye kalenda ya FI ikiwa na mashabiki wengi wenye moyo. FIA inatarajia mbio hizo za China zitafanyika mapema iwezekanavyo na kuwatakia kila heri watu wote katika kipindi kigumu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |