• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Real Sociedad wataka dau nono kuwamchia William Jose kwenda Barcelona, Chelsea waja na ofa ya pound m 38 kumpata Ziyech

  (GMT+08:00) 2020-02-13 08:15:52

  Klabu ya FC Barcelona kwa sasa ina wakati mgumu kufuatia kuumia kwa mshambuiaji wao Ousmane Dembele ambaye amefanyiwa upasuaji na atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 6. Kufuatia kuumia huko FC Barcelona wanataka kumsajili William Jose kutoka Real Sociedad kama mbadala sahihi wa Dembele lakini Real Socoedad wanataka dau kubwa ili kuidhinisha dili hilo. Kocha wa Real Sociedad Imanol ameweka wazi kuwa mchezaji huyo anaweza kuondoka kwa euro milioni 70, kocha huyo inadaiwa katoa kauli hiyo kutokana na kipengele kilichopo katika mkataba wa mchezaji huyo kuwa euro milioni 70 zinaweza kuvunja mkataba wake. Kwa upande wa EPL klabu ya Chelsea ya England sasa imejipanga kuhakikisha inaboresha safu yake ya kiungo kwa kukamilisha usajili wa Hakim Ziyech kutokea Ajax ya Uholanzi. Awali inadaiwa kuwa Chelsea walitaka kumsajili Hakim,26, dirisha dogo la Januari lakini Ajax walikataa na kusema wako radhi kumuachia mwisho wa msimu. Chelsea wapo mezani na Ajax kwa sasa wakiwa na ofa nono ya pound milioni 38 zaidi ya Tsh bilioni 100 kwa ajili ya kujihakikishia kuwa mwisho wa msimu nyota huyo anakuwa wao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako