• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Walipa kodi wa Kenya wataka serikali iondoe misamaha ya kodi kwa makampuni ya kigeni

  (GMT+08:00) 2020-02-13 09:24:30

  Jumuiya ya walipa kodi ya Kenya (NTA) imeitaka serikali kuondoa misamaha ya kodi inayotolewa kuvutia makampuni ya kigeni, ikiwa ni njia ya kuongeza mapato.

  Mratibu wa taifa wa jumuiya hiyo Bibi Irene Otieno amesema utafiti umeonyesha kuwa mazingira mazuri ya biashara, yakiambatana na usalama wa kutosha na gharama nafuu za nishati vinatosha kuvutia wawekezaji wageni.

  Bibi Otieno amesema sababu inayofanya Kenya ishindwe kufikia malengo ya makusanyo ya kodi, ni misamaha mbalimbali. Pia amesema misamaha ya kodi inawafanya wajasiriamali wenyeji kuwa kwenye nafasi isiyo na manufaa ikilinganishwa na wawekezaji wageni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako