• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanaharakati wa Kenya wataka kuwe na elimu ya lugha ya ishara mashuleni

  (GMT+08:00) 2020-02-13 09:24:51

  Wanakampeni wa Kenya wameitaka serikali kuweka mafunzo ya msingi ya lugha ya ishara kwenye shule ili kuhimiza mawasiliano na watu wenye ulemavu.

  Mwanzilishi wa jumuiya ya wenye ulemavu ya Kenya Bibi Jemimah Kutata, amesema Kenya inahitaji watu wenye ujuzi wa elimu rasmi ya ishara ili kusaidia kupambana na ubaguzi unaowakabili wanawake na wasichana wenye ulemavu.

  Amesema kupata huduma ni changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu, na wanaitaka serikali itoe watafsiri kwenye shule, hospitali na maeneo ya umma ili kuwe na mawasiliano na watoa huduma. Bibi Kutata amesema waandaaji wa shughuli mbalimbali wanatakiwa kuwafikiria watu wenye ulemavu wanapoandaa matukio ili waweze kufika majukwaani, kutumia vyoo na ngazi kwa urahisi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako