Idadi ya hospitali zilizoteuliwa kuwapokea wagonjwa wa nimonia ya COVID-19 inayosababishwa na virusi vipya vya korona mjini Wuhan, imezidi 40.
Kwa mujibu wa makao makuu ya udhibiti wa mlipuko wa virusi hivyo mjini Wuhan, vitanda vyote 12,000 katika hospitali zilizoteuliwa na hospitali mbili za muda mjini humo, vitatumiwa kutoa matibabu kwa wagonjwa wa virusi hivyo walio katika hali mbaya na mahututi.
Mji wa Wuhan kwa sasa umeweka hospitali saba za muda kwenye majumba ya michezo na ya maonesho, ambazo zina wafanyakazi 4,966 wa matibabu na zimepokea wagonjwa 3,972.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |