• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping aongoza mkutano wa kamati ya kudumu ya ofisi ya siasa ya kamati kuu ya CPC kuhusu udhibiti wa mlipuko wa virusi vya korona

  (GMT+08:00) 2020-02-13 09:38:50

  Kamati ya kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China jana Jumatano ilikutana ikisikiliza ripoti kutoka kwa kikundi cha uongozi cha kukabiliana na mlipuko wa virusi vya korona, kuchambua hali ya sasa ya mlipuko huo na kujadili namna ya kuimarisha kazi ya udhibiti. Rais Xi Jinping ameongoza mkutano huo na kutoa hotuba muhimu.

  Rais Xi amesisitiza kuwa sasa kazi ya kudhibiti mlipuko wa virusi hivyo imefikia kipindi muhimu, na idara husika zinatakiwa kufanya kila juhudi katika kazi ya udhibiti, hasa kwenye maeneo yaliyoathiriwa vibaya na yenye hatari kubwa.

  Mkutano huo umeziagiza idara husika kuinua zaidi kiwango cha kuwapokea na kuwatibu wagonjwa, na kupunguza kiwango cha maambukizi na vifo, na pia kuhakikisha ugavi wa vifaa vya matibabu, na kupanua uzalishaji wa mask na nguo za kujikinga, ili kukidhi mahitaji ya mapambano dhidi ya virusi hivyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako