• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu na watunga sera wa Afrika watoa mwito wa kuweka sera wezeshi ili kuhimiza maendeleo ya Afrika

    (GMT+08:00) 2020-02-13 09:50:04

    Wataalamu na watunga sera wa Afrika wanaohudhuria baraza la biashara la Afrika wamesisitiza kuwa nchi za Afrika zinaweza kutimiza ongezeko kubwa la uchumi kwa kufuata utawala bora na kuweka sera wezeshi kwa mtaji binafsi kuingia katika sekta za nishati, afya na Tehama.

    Wataalamu hao wametoa mwito wa kuhimiza utawala bora kwenye mkutano wa tatu wa baraza la biashara la Afrika ABF-2020, ulioandaliwa na kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa UNECA mjini Addis Ababa, chini ya kauli mbiu ya "Kuwekeza katika watu, sayari na ustawi".

    Mkutano huo umehudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Afrika, wakiwemo rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, waziri mkuu wa Msumbiji Carlos Agostinho do Rosario pamoja na mawaziri na wawekezaji wengine, ambao wamebadilishana maoni kuhusu utoaji fedha wenye ubunifu katika sekta za nishati, afya na Tehama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako