• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Russia yailaani Uturuki kuharibu Makubaliano ya Sochi

  (GMT+08:00) 2020-02-13 09:53:13

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Russia Bibi Maria Zakharova amesema Uturuki kutotekeleza makubaliano yaliyofikiliwa na viongozi wa Russia walipokutana mjini Sochi mwaka 2018, ni sababu kuu inayosababisha hali ya wasiwasi izidi kuwa mbaya kaskazini mwa Syria.

  Bibi Zakharova amesema Uturuki imetuma jeshi kaskazini mwa Syria, kitendo ambacho kimeharibu Makubaliano ya Sochi na kusababisha hali ya wasiwasi mkoani Idlib izidi kuwa mbaya. Amesema Russia inapenda kuendelea kufanya mazungumzo na Uturuki juu ya kutuliza hali ya mkoa wa Idlib.

  Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kama askari wa Uturuki walioko vituo vya uchunguzi huko Idlib watashambuliwa tena, Uturuki itafanya mashambulizi kutoka mahali popote dhidi ya jeshi la serikali ya Syria bila ya kujali Makubaliano ya Sochi.

  Wakati huohuo, mjumbe maalumu wa Marekani nchini Syria Bw. James Jeffrey amekutana na naibu waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Bw. Sedat Onal na msemaji wa rais wa Uturuki Bw. Ibrahim Kalin, ambao wamejadili suala la maendeleo ya hali ya Syria pamoja na juhudi zinazofanywa kwa ajili ya kuhimiza utulivu na usalama nchini Syria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako