Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bibi Kristalina Georgieva, amesema serikali ya China imechukua hatua mwafaka katika kuzuia na kudhibiti mlipuko wa virusi vya korona vinavyosababisha nimonia ya COVID-19, na kwamba sasa bado ni mapema kutathmini athari za mlipuko wa virusi hivyo kwa uchumi wa China.
Bibi Georgieva amesema IMF inapongeza serikali ya China kwa kuchukua hatua shirikishi katika sehemu zinazoathiriwa vibaya na mlipuko wa virusi vya korona, na kupashana habari na Shirika la afya duniani WHO na jumuiya ya kimataifa. Pia amesema China ina bajeti ya kutosha katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo, na IMF inaona ni sawa kwa serikali ya China kutochukua hatua kwa haraka kuchochea uchumi. Vilevile ameeleza kuwa uzalishaji viwandani umeanza kurejeshwa hatua kwa hatua, ndiyo maana bado haujafikia wakati wa kutathmini athari za mlipuko wa ugonjwa huo kwa uchumi wa China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |