Mbali na kutaka kuiletea Tanzania medali ya tatu yam bio za kimataifa za Lake Biwa marathon, mwanariadha Alphonse Simbu amesema atazitumia mbio hizo kuboresha muda wake kabla ya kwenda kwenye Olimpiki. Simbu ni miongoni mwa wanariadha nyota wa dunia wa marathoni wanaotarajiwa kuchuana katika mbio hizo za 75 zitakazofanyika Machi 8 mjini Osaka, Japan. Mshindi huyo wa medali ya shaba katika mashindano yam waka 2017, amesema matokeo yam bio hizo yatampa mwongozo na kumpima kikamilifu kuelekea michezo ya Olimpiki ya Tokyo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |