• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mo Farah sio tishio tena, yasema AK

  (GMT+08:00) 2020-02-13 17:05:56

  Kocha wa timu ya taifa katika Shirikisho la Riadha Kenya (AK), Julius Kirwa, amesema kurejea kwa nyota Mo Farah katika mbio za mita 10,000, hakutayumbisha matumaini ya Kenya kutawala fani hiyo kwenye Olimpiki za 2020 jijini Tokyo. Mo Farah wa Uingereza ndiye mkimbiaji anayejivunia ufanisi mkubwa zaidi katika ulingo wa riadha. Amethibitisha kwamba atashuka ugani kuwania medali ya dhahabu katika mbio za mita 10,000 jijini Tokyo. Hii ni licha ya kustaafu miaka miwili iliyopita na kujibwaga katika mbio za masafa marefu za marathon, ambako hajafanikiwa, huku akiambulia nafasi ya nane katika Chicago Marathon mwishoni mwa mwaka uliopita. Michezo ijayo ya Olimpiki itampa Farah nafasi maridhawa ya kujizolea nishani ya 11 ya dhahabu katika historia yake ya mbio za 10,000. Farah, 36, anajivunia dhahabu nne za Olimpiki baada ya kutawala mbio za mita 5,000 na 10,000 katika makala yaliyopita ya London, Uingereza (2012) na Rio, Brazil (2016).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako