• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Bayern itanyoa Chelsea katika Uefa – Ballack

  (GMT+08:00) 2020-02-13 17:06:14

  Aliyekuwa kiungo mahiri wa Bayern Munich, Michael Ballack, anapigia upatu mabingwa hao wa Ujerumani kutinga robo-fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA). Ballack alipata ufanisi mkubwa akichezea Bayern na pia Chelsea ya Uingereza. Klabu zake hizo mbili za zamani zitakutana kwa mechi ya mkondo wa kwanza katika raundi ya 16 ya UEFA, itakayochezewa ugani Stamford Bridge, Jumanne ijayo. Ballack asema Bayern ina nafasi kubwa dhidi ya wapinzani wao, ambao wananolewa na rafiki yake mkubwa Frank Lampard. Chelsea, ambao walimaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi H, nyuma ya Valencia, walifanikiwa kusonga mbele baada ya kupiku Ajax, waliotinga nusu-fainali msimu uliopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako