• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China aagiza kupeleka madaktari wengine 2,600 wa jeshi katika mji wa Wuhan unaokumbwa na maambukizi

  (GMT+08:00) 2020-02-13 18:25:06

  Rais Xi Jinping wa China ameagiza madaktari wengine 2,600 wa kijeshi kupelekwa wametumwa mjini Wuhan, ambao umeathirika zaidi na maambukizi ya virusi vipya ya korona COVID-19.

  Madaktari hao watahudumia wagonjwa katika Hospitali ya Taikangtongji na Hospitali ya Wanawake na Watoto wa Mkoa wa Hubei, kama wenzao wanavyofanya katika Hospitali ya Huoshenshan.

  Mpaka sasa, madaktari zaidi ya 4,000 kutoka majeshi ya China wamepelekwa mjini Wuhan, na madaktari hao wapya wanatoka jeshi la nchi kavu, jeshi la majini, jeshi la angani, jeshi la makombora na jeshi la misaada ya kimkakati.

  Rais Xi ameahidi kufanya juhudi zote ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,300. Amesisitiza kuwa, wanajeshi lazima wakumbuke majukumu yao, na kubeba wajibu wa kutoa mchango kwa kushinda vita dhidi ya maambukizi hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako