• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wakubali kupeleka ujumbe wa kisiasa nchini Sudan

    (GMT+08:00) 2020-02-13 18:26:56

    Sudan imesema Umoja wa Mataifa umekubali ombi lake la kutuma ujumbe wa kisiasa nchini humo kwa ajili ya kusaidia serikali ya mpito ya Sudan, na kuunga mkono idara mbalimbali za nchi hiyo kupata maendeleo endelevu.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Sudan imesema, waziri wa wizara hiyo Bw. Omar Gamar-Eddin Ismail jana amekutana na naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya siasa na amani Bibi Rosemary DiCarlo mjini Khartoum. Gamar-Eddin amesema Sudan na Umoja wa Mataifa zimefikia makubaliano ya kutuma ujumbe maalumu wa kisiasa nchini humo, ili kusaidia serikali yake kujenga amani. Ujumbe huo utakuwepo nchini humo mpaka muda wa miezi 39 wa serikali ya mpito ya Sudan umalizike.

    Gamar-Eddin amesisitiza tena kuwa serikali ya Sudan imeahidi kushirikiana na kanda na jumuiya ya kimataifa katika muda wa mpito, na kutimiza matumaini ya wananchi wake juu ya uhuru, amani, haki na usawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako