• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la China halikushiriki kwa namna yoyote ya kuiba siri kwenye mtandao wa inteneti

    (GMT+08:00) 2020-02-13 18:28:10

    Wizara ya sheria ya Marekani hivi karibuni ilitangaza kuwashtaki wanajeshi wanne wa China ikidai kuwa wanahusika na kufanya udukuzi dhidi ya idara ya kutoa ripoti ya dhamana ya Marekani.

    Akizungumzia hilo, msemaji wa wizara ya ulinzi ya China Bw. Wu Qian amesema, mashtaka ya Marekani hayana msingi halisi na ni kitendo cha umwamba na uonevu wa utekelezaji wa sheria, na China inapinga na kulaani vikali kitendo hicho. Amesema China inalinda usalama wa kimataifa wa inteneti, na daima serikali ya China inapinga na kupambana na uhalifu wa mtandaoni. Amesisitiza kuwa, jeshi la Chiba halihusiki na shughuli za aina yoyote za kuiba siri kwenye mtandao wa inteneti.

    Bw. Wu Qian ameitaka Marekani irekebishe kosa na kufuta mashtaka, ili kuepuka kuharibu uhusiano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako