Mjumbe wa kudumu wa Kenya kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO) Bw. Rudi Eggers amesema, hatua zilizochukuliwa na China katika kupambana na maambukizi ya virusi vipya vya korona COVID-19 ni za haraka na wazi.
Mjumbe huyo amesema, hali ya maambukizi ya virusi hivyo inaelekea kutulia kutokana na kupungua kwa kasi ya ongezeko la watu walioambukizwa virusi hivyo duniani na nchini China. Amesema China ilichukua hatua za haraka na wazi kwa kupambana na virusi hiyo, ambazo zimesifiwa na jumuiya ya kimataifa.
Aidha amesema, Kenya, Afrika Kusini na Ethiopia zinakabiliana na tishio kubwa la kuenea kwa COVID-19, na nchi za Afrika zinapaswa kuwaelimisha watu wake kuhusu ugonjwa huo, ili kuwaondolea wasiwasi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |