• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NATO kupanua kazi ya mafunzo kwa jeshi la Iraq

  (GMT+08:00) 2020-02-13 18:28:58

  Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wamekubaliana kupanua muungano wa mafunzo wa NATO nchini Iraq, ikiwa ni kujibu amri ya rais wa Marekani Donald Trump kwa jumuiya hiyo kufanya kazi zaidi katika Mashariki ya Kati.

  Katibu Mkuu huyo amesema NATO itachukua baadhi ya maeneo ya mafunzo yanayofanywa na muungano unaongozwa na Marekani dhidi ya kundi la ISIL.

  Majukumu ya NATO na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani nchini Iraq yamesitishwa kutokana na hali tete ya usalama katika kanda hiyo baada ya ndege isiyo na rubani ya Marekani kufanya shambulizi lililomuua kamanda wa ngazi ya juu wa Iran mwanzoni mwa mwezi uliopita.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako