• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa wito kwa pande zote husika zitekeleze matokeo ya mkutano wa kilele wa Berlin juu ya suala la Libya

  (GMT+08:00) 2020-02-13 18:29:53

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limepitisha Azimio namba 2510 kukubali matokeo ya mkutano wa kilele wa Berlin juu ya suala la Libya.

  Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema, China inataka pande zote husika zitekeleze kwa makini matokeo ya mkutano huo. Amesema hali ya sasa ya Libya yenye utatanishi inaathiri vibaya usalama na utulivu wa nchi jirani na kikanda. China inaunga mkono Umoja wa Mataifa uendelee kufanya kazi ya uongozi, na inatoa wito kwa pande zote zinazopingana nchini Libya wa kusimamisha vita haraka iwezekanavyo. Balozi Wu amesema China inapongeza hatua za kiujenzi zilizochukuliwa na jumuiya ya kimataifa hivi karibuni katika kupunguza mvutano nchini Libya.

  Wu ameongeza kuwa China inaunga mkono Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zifanye kazi zao za pekee katika kutatua suala la Libya kwa njia ya kisiasa. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuwa makini na aina zote za ugaidi kwenye mchakato wa kutimiza amani nchini Libya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako