• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani yarejesha ufadhili kwa Somalia ili kuboresha juhudi za nchi hiyo kupambana na ugaidi

  (GMT+08:00) 2020-02-13 18:59:16

  Marekani imerejesha tena baadhi ya msaada wake wa kiusalama kwa Somalia ili kusaidia operesheni za kupambana na ugaidi nchini humo dhidi ya kundi la al-Shabaab.

  Marekani, ambayo mwaka 2017 ilisitisha msaada wa chakula na mafuta kwa vikosi vingi vya jeshi la Somalia kutokana na wasiwasi wa ufisadi, imepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya Somalia kuboresha usimamizi wa taasisi za umma za kifedha za Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo.

  Marekani imeitaka serikali ya Somalia kuendelea kutoa kipaumbele kwa mageuzi ya sekta ya usalama, ikiwemo usimamizi wa mali na rasilimali watu, kama sehemu ya juhudi za kina za kujenga na kudumisha vikosi vya usalama vya kitaaluma, vyenye uwezo, na vinavyowajibika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako