• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mlipuko wa COVID-19 ni kipimo cha urafiki kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2020-02-13 19:03:13

    Vita ya dunia dhidi ya mlipuko wa virusi vipya vya korona COVID-19 imekuwa kipimo muhimu cha urafiki wa kudumu kati ya China na nchi za Afrika. Kwa muda mrefu China imekuwa mchangiaji mkubwa katika kudumisha afya ya umma kote duniani, haswa barani Afrika. Katika miongo mitano iliyopita, China imepeleka madaktari 21,000 barani Afrika, ambao wamewatibu zaidi ya wagonjwa milioni 200 barani humo.

    Baada ya kutokea kwa mlipuko wa virusi vya Ebola barani Afrika mwezi Machi mwaka 2014, baadhi ya nchi zilifunga balozi zao na kuwaondoa wanadiplomasia na raia wao kutoka nchi tatu za Afrika Magharibi zilizoathiriwa sana na janga hilo. Katika wakati huo mgumu, China iliamua kubaki katika nchi hizo na kutoa msaada. Serikali ya China sio tu ilituma misaada iliohitajika kwa dharura, bali pia timu ya madaktari 1,000 wa kijeshi na kiraia katika maeneo yalioathirika zaidi na ugonjwa huo. Wanadiplomasia na wataalam wa matibabu wa China walipambana kwa pamoja na janga hilo kwa kushirikiana na wakaazi wa eneo hilo hadi mlipuko huo ulipodhibitiwa.

    Hali ngumu hubaini urafiki wa kweli, na urafiki kati ya China na Afrika umehimili majaribio mbalimbali. Katika Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika uliomalizika Jumatatu wiki hii huko Addis Ababa, Ethiopia, viongozi wa nchi wanachama wa Umoja huo walielezea mshikamano wao na imani na serikali ya China pamoja na watu wake katika juhudi zao za kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

    Serikali za nchi za Afrika na watu wao pia wameiunga mkono kithabiti China kupitia njia mbali mbali. Comoros, ambayo ni moja ya nchi zilizo nyuma kimaendeleo barani Africa, imechangia dola 109 kwa China kupambana na COVID-19, ambayo ni dalili ya nia yake ya kuiunga mkono China. Kufikia sasa, Afrika bado haijapata kesi yoyote ya virusi vya korona, ikizingatiwa kuwa na bara hilo limekuwa likifuata ushauri wa Shirika la Afya Duniani WHO kwamba, haipaswi kuwa na kizuizi cha safari za ndege kwenda au kutoka China.

    Huku sasa dunia ikikabiliwa na mgogoro wa afya ya umma, kulaumiana au kuwa na hofu hakutasaidia kushinda mapambano dhidi ya virusi vipya vya korona. Kazi kubwa kwa kila mtu sasa ni kushinda mapambano hayo kwa kushikamana kwa pamoja.

    Tukumbuke kuwa milipuko ya magonjwa kama vile Ebola imeshindwa kupitia juhudi zilizoratibiwa, hivi karibuni, rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Tijjani Muhammad-Bande, ametoa wito wa mshikamano na ushirikiano wa aina tofauti katika nyakati za shida.

    Ili kumaliza janga hilo haraka iwezekanavyo, China imefanya bidii za pande zote kuwahudumia waathiriwa na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Lakini China pekee haiwezi kupata mafanikio, inahitaji juhudi za pamoja na msaada kutoka kwa jamii ya kimataifa.

    China inashukuru kwa misaada kutoka kote duniani, na itaendelea kutoa habari kwa wote, na kuimarisha ushirikiano na nchi nyingine kwa njia wazi na inayowajibika, ili kulinda maisha na afya za watu wa China, na kuchangia kuboresha afya ya umma ya kikanda na duniani.

    Katika umoja, kuna nguvu. Kwa taratibu lakini kithabiti, hatimaye watu watashinda ugonjwa huu hatari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako