• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabishara watakiwa kufanya kazi na taasisi ya viwango vya ZBS

    (GMT+08:00) 2020-02-13 19:38:47

    Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar,balozi Amina Salum amesema ni wajibu kwa wafanyabisahara kufanya kazi zao kwa karibu na taasisi ya viwango ZBS ili kuinusuru nchi kuwa ghala za bidhaa zisizo na viwango vya ubora.

    Balozi Salum ametoa tamko hilo wakati akifungua mkutano wa majadiliano uliowashirikisha wafanyabiashara na ZBS juu ya umuhimu wa viwango vya ubora.

    Amesisitiza kuwa wafanyabishara wana dhamana kubwa ya kuwalinda walaji na watumiaji wa bidhaa zinazozalishwa nchini humo na zile zinazoagizwa kutoka nje ya nchi kwa kuweka mkazo zaidi katika matumizi ya viwango vinavyoandaliwa kitaalamu na ZBS kwani vitawasaidia kuhimili ushindani wa soko.

    Mkurugenzi wa usimamizi Rahima Bakari amesema tayari ZBS imeidhinisha viwango vya ubora 290 katika bidhaa tofauti na kuwahimiza wafanyabiashara kuvitumia ipasavyo ili kuwa na uhakika wa biashara zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako