• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sheria kurahisishwa ili kuvutia wawekezaji

  (GMT+08:00) 2020-02-13 19:39:53
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji, Angellah Kairuki, amesema serikali inafanya mapitio ya sheria ya uwekezaji ili kukidhi mahitaji ya sasa na kuvutia wawekezaji.

  Aidha, ameshauri benki ziwekewe masharti ili zitoe mikopo katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.

  Kairuki alisema hayo jana alipokuwa akifungua kongamano la sita la Jukwaa la Wadau wa Sera za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, jijini hapa kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

  Alisema serikali imedhamiria kuimarisha uwekezaji kwenye kilimo, mifugo na uvuvi kwa kuwa ni sekta zitakazoifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Pia waziri huyo alisema wameanza kufanyia kazi kuwa na vivutio maalum kwa mkoa wa Dodoma ili kupata wawekezaji wengi zaidi.

  Alisema wameamua kuimarisha uchumi wa nchi kupitia sekta ya viwanda, kilimo ndio msingi mkuu wa maendeleo ya viwanda.

  Alisema Sekta hizi zinategemeana na ukuaji wa pamoja kilimo na viwanda, asilimia 65 ya malighafi nchini Tanzania inatokana na sekta ya kilimo.

  Alibainisha kuwa kwa mwaka 2018, miradi 2821 ilisajiliwa na kituo cha uwekezaji na asilimia 17.9 ya miradi ni ya kilimo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako