• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KRA kuanza kukusanya ushuru mapema

  (GMT+08:00) 2020-02-13 19:40:11

  Makampuni na watu binafsi nchini Kenya hivi sasa wataanza kulipa ushuru mwanzo wa mwaka wa kifedha kila tarehe 1 Julai iwapo wabunge wataidhinisha muswada pendekezi ambao unasubiri kupitishwa kuwa Sheria ya Fedha ili kushughulikia ucheleweshwaji katika ukusanyaji wa ushuru ambao umeathiri malengo ya Mamlaka ya ukusanyaji Mapato (KRA).

  Sheria ya Biashara 2019,inahitaji Hazina ya Taifa kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Fedha bungeni kabla ya tarehe 30 Aprili ili iweze kupitishwa na Rais kama sheria kufikia tarehe 30 Juni.

  Hii ni kuondokana na mfumo wa sasa ambapo muswada wa fedha unawasilishwa Bungeni baada ya wiki ya tatu ya mwezi Juni na inachukua miezi kabla ya kuwa sheria.

  Kuchelewa huko kunatajwa kuathiri ukusanyaji wa ushuru,jambo lilofanya kuwa vigumu kwa Mamlaka ya Mapato nchini Kenya (KRA) kufikia malengo yake ya ukusanyaji ushuru,na kusababisha mabadiliko ya mara kwa mara kwa Bajeti ya Taifa ili iweze kukidhi kiwango kidogo cha ukusanyaji ushuru.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako