• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chuo kikuu binafsi nchini Kenya chazindua darasa la Confucius ili kuhimiza mafunzo ya lugha ya Kichina

    (GMT+08:00) 2020-02-14 09:32:34

    Chuo kikuu binafsi cha USIU-Africa nchini Kenya jana Alhamisi kilizindua darasa la Confucius kwa lengo la kuimarisha mafunzo ya lugha ya Kichina kwa wanafunzi na walimu.

    Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Mtaala nchini Kenya KICD Bw. Julius Jwan, amesema darasa la Confucius ambalo ni la kwanza kuzinduliwa katika chuo kikuu binafsi nchini litasaidia kuhimiza elimu ya lugha ya Kichina miongoni mwa vijana, na kwamba Kenya inapanga kuzindua somo ya lugha ya Kichina kama somo la kuchagua kuanzia darasa la nne.

    Darasa hilo la Confucius la USIU-Africa lilianzishwa kwa ushirikiano na taasisi ya Confucius katika Chuo kikuu cha Kenyatta, ili kusaidia kupanua mafunzo ya lugha ya Kichina na utamaduni kwa vijana wa Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako