• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kuwaita vijana wa NYS kupambana na nzige wa jangwani

  (GMT+08:00) 2020-02-14 09:32:50

  Kenya inapanga kuwaita vijana waliopewa mafunzo katika Shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa NYS, ili kuimarisha mapambano dhidi ya nzige wa jangwani waliovamia kaunti 17 nchini humo.

  Katibu msimamizi katika Idara ya Taifa ya Mazao ya Kilimo Bw. Kello Harsama amesema vijana 600 waliopewa mafunzo wataitwa kupitia ushirikiano na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, kushiriki kwenye kazi ya kupuliza dawa za kuua nzige kutoka ardhini.

  Akiongea kwenye Jukwaa la mafunzo kwa vijana mjini Naivasha, Bw. Harsama amesema wanawashirikisha vijana wa NYS ili kuimarisha mapambano yanayoendelea dhidi ya nzige wa jangwani, ambao uvamizi wao umeleta tishio kubwa kwa usalama wa chakula nchini Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako