• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • OLIMPIKI: Olimpiki ya Tokyo kutoahirishwa kwasababu ya COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-02-14 09:44:51

    Waandaaji wa Olimpiki ya Tokyo wamesisitiza jana kuwa hawafikirii kuahirisha michezo kutokana na virusi vya korona na kukanusha uvumi kwamba wanampango wa kuahirisha. Zikiwa zimesalia siku 161 tu hadi sherehe ya ufunguzi, kumezuka wasiwasi kuhusu Japan kuandaa michezo huku virusi vikizi kuenea katika Adia nzima. Lakini Mkurugenzi Mkuu wa Tokyo 2020 Yoshiro Mori ameondoa wasiwasi huo kwenye mkutano na maofisa wa ngazi ya juu wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa. Wakati huohuo michuano ya raga kwa wachezaji saba ya Hong Kong na Singapore jana iliahirishwa kutoka April hadi hadi Oktoba kutokana na virusi hivyo, wakijiunga na China Grand Prix, gofu na soka kwenye orodha ya michuano iliyoahirishwa. Umuzi huo ambao utaingilia kati timu za raga ya wachezaji saba zitakazofanikiwa kucheza Olimpiki ya Tokyo, umetolewa kutokana wasiwasi wa mlipumo wa COVID-19. Michuano ya raga ya Hong Kong ilipangwa kufanyika tarehe 3-5, na wiki moja baadaye kuanza kwa michuano ya Singapore.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako