Benki ya Dunia imeahidi kuunga mkono Afrika kupanua mkopo kwa makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati. Mtaalamu wa sekta ya fedha wa Benki ya Dunia Bibi Luz Maria Salamina, amesema hayo kwenye mkutano wa baraza la mkopo uliofanyika huko Nairobi, na akiongeza kuwa upatikanaji wa fedha kwa makampuni hayo ukiwa nguvu ya msukumo kwa ukuaji wa uchumi, bado ni changamoto kuu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |