• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Joseph Yobo atajwa kuwa kocha msaidizi mpya wa Nigeria

  (GMT+08:00) 2020-02-14 09:45:35

  Nahodha wa zamani wa Nigeria na Everton mshambuliaji Joseph Yobo ametajwa kuwa kocha msaidizi mpya wa Nigeria na Shirikisho la Soka la (NFF) Yobo, mwenye miaka 39, amechukua nafasi ya Imama Amapakabo, aliyemsaidia kocha mkuu Gernot Rohr wakati Salisu Yusuf alipofungiwa mwaka jana kwa kupokea pesa kutoka kwa wanahabari wapelelezi waliojifanya kama mawakala. Yobo ameisaida Super Eagles kuchukua Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 na kuingia hatua ya 16 bora kwenye Kombe la Dunia mwaka 2014. Yobo amecheza mara 258 kwenye timu ya Everton na pia alicheza Standard Liege, Marseille na Fenerbahce.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako