Kombora la aina ya Katyusha limeanguka kwenye kituo cha jeshi la Marekani katika mkoa wa Kirkuk, kaskazini mwa Iraq. Shambulizi hilo lilitokea jana jioni bila kusababisha kifo au majeruhi. Kikosi cha polisi cha Iraq kimefanya usakaji eneo lilikorushwa kombora hilo, na kugundua kifaa cha kurushia makombora chenye makombora kumi na mbili, kombora moja tu likiwa limerushwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |