• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yakaribisha uamuzi wa bunge la Ujerumani kurejesha uhusiano kati ya nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2020-02-14 09:46:06

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Sudan inasema serikali ya nchi hiyo imekaribisha uamuzi wa bunge la Ujerumani kurejesha na kupanua uhusiano wa kiuchumi na kimaendeleo kati ya nchi hizo mbili baada ya miongo mitatu.

    Taarifa pia inasema uamuzi huo umetolewa ikiwa ni sehemu ya makubaliano kati ya Ujerumani na Sudan kufuatia mafanikio ya mapinduzi, wakati serikali ya Ujerumani ikituma ujumbe wa kiserikali na wa kiufundi kuunga mkono mahitaji ya kipindi hiki kwa mujibu wa mambo yanayopewa kipaumbele na serikali ya mpito.

    Bunge la Ujerumani lilifanya uamuzi wa kusimamisha ushirikiano wa maendeleo na Sudan mwaka 1989, kutokana na kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako