• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Odion Ighalo afanya mazoezi mbali na kambi ya United

  (GMT+08:00) 2020-02-14 09:46:52

  Mchezaji mpya wa Manchester United ambaye ametoka kusainiwa hivi majuzi Odion Ighalo anafanya mazoezi mbali na kambi ya United wiki hii ikiwa ni kama hatua za tahadhari kufuatia kwenda Uingereza akitokea China. United imeamua kumuwekea karantini kwasababu ya hatari inayotokana na virusi vya korona. Wameamua kutomchukua mshambuliaji huyo kwenye kambi yao ya mazoezi ya majira ya baridi nchini Hispania kwasababu ya wasiwasi anaweza kupata ugumu kurudi Uingereza. Ighalo, mwenye miaka 30, anatarajiwa kusafiri na kikosi chake kipya kwenye mechi ya Jumatatu dhidi ya Chelsea. Ighalo amekuwa akifanya mazoezi kwenye kituo cha Taifa cha Taekwondo, karibu na Uwanja wa Etihad mahali ambapo amekuwa akikaa tangu awasili nchini Uingereza siku 12 zilizopita. Ighalo amejiunga na United kwa mkopo kwa msimu wote uliosalia akitokea Ligi kuu ya China katika klabu ya Shanghai Shenhua. Ushauri uliopo sasa ni kwamba wasafiri wanaokwenda Uingereza wakitokea nchi maalumu ikiweno China, wanawekewa karantini ya siku 14.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako