• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kocha Steven Ludwig aonywa na refa Kassim Mpanga afungiwa miezi mitatu

  (GMT+08:00) 2020-02-14 09:47:52

  Kocha wa Simba SC, Steven Ludwig Vandenbroeck amepewa onyo kali kwa kosa la kugoma kuwafungulia mlango mwamuzi na Kamishina wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga Februari 1, mwaka huu Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa Vyombo vya Habari imesema adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya Ligi Kuu ya Udhibiti wa Makocha. Naye refa msaidizi namba mbili, Kassim Mpanga amefungiwa miezi mitatu kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu katika mechi kati ya Simba SC na JKT Tanzania Februari 7 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako