Mkuu wa Hospitali ya Jinyintan ya Wuhan nchini China Bw. Zhang Dingyu jana amezungumza na wanahabari akitoa wito kwa wagonjwa waliopona baada ya kuambukizwa virusi vya korona (COVID-19) wajitolee damu, kufuatia chembechembe za kinga kugunduliwa kwenye damu ya baadhi ya wagonjwa.
Bw. Zhang amesema uchunguzi wa awali umethibitisha kuwa matibabu ya kutumia plasma ya damu ya wagonjwa waliopona kwa wagonjwa walioambukizwa virusi vya COVID-19 yanafanya kazi.
Idara ya afya ya China imesema hadi kufikia Jumatano wiki hii, wagonjwa 5,911 kwa ujumla waliruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupona, 1,171 kati yao waliondoka hospitali Jumatano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |