Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ameitisha mkutano wa kikundi cha uongozi cha kupambana na virusi vya Korona, na kueleza kuwa sehemu na idara mbalimbali zinapaswa kutekeleza maagizo muhimu yaliyotolewa na rais Xi Jinping na maamuzi yaliyofikiwa ya mikutano ya Ofisi ya Siasa ya Kamati kuu ya Chama, kuonesha nia thabiti katika kushinda vita dhidi ya ugonjwa huo, na kujitahidi kutimiza malengo ya maendeleo ya uchumi na jamii kwa mwaka huu.
Mkutano huo pia umesisitiza kutoa kipaumbele katika kazi ya kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo mkoani Hubei, haswa katika mji wa Wuhan. Pia imeelezwa kuwa utaratibu wa pamoja wa kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo wa baraza la serikali unapaswa kuhakikisha upatikanaji wa vifaa na nguvu kazi kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo, kusaidia utatuzi wa matatizo makuu na kutangaza kwa wakati habari zinazohusika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |