• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza kushirikiana na Malaysia katika kupambana na mlipuko wa virusi vya korona COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-02-14 10:02:51

    Rais Xi Jinping wa China jana alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Malaysia Bw. Mahathir Mohamad, na kusema nchi zao zinatakiwa kushirikiana kupambana na mlipuko wa virusi vya korona COVID-19, huku zikihimiza ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja uzae matunda mengi zaidi ili kuzinufaisha nchi zao.

    Kwa upande wake Bw. Mahathir amepongeza juhudi za China na maendeleo mapya yaliyopatikana katika kupambana na ugonjwa huo, akiona kuwa huu ni mchango wa China ikiwa nchi kubwa inayowajibika kulinda usalama wa umma wa dunia. Malaysia imetoa vifaa vya matibabu kwa China na kupenda kuendelea kutoa misaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako