• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Benki ya Standard Chartered na Tanzania zasaini makubaliano kuhusu mradi wa SGR

  (GMT+08:00) 2020-02-14 10:24:36

  Wizara ya fedha na mipango ya Tanzania imesaini makubaliano na benki ya Standard Chartered kuhusu mkopo wa dola za kimarekani bilioni 1.46 kwa mradi wa reli ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora mjini Dodoma.

  Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema, reli hiyo ya SGR inayounganisha Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma ina urefu wa kilomita 550, ambayo ni mradi mkubwa zaidi nchini humo.

  Waziri wa fedha na mipango wa Tanzania Bw. Philip Mpango amesema. chini ya msaada wa benki ya Standard Chartered na washirika wengine, mkopo wa mradi huo utaongeza ajira za moja kwa moja nchini Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako